Kwa kuchapisha maudhui kwenye Airbnb, unakubali kufuata sera hii. Maudhui yanajumuisha maudhui yoyote ya maandishi, picha, sauti, video au mengine, ikiwemo:
Tuna haki ya kuondoa maudhui yoyote, yote au kwa sehemu, ambayo yanakiuka sera hii, Masharti yetu ya Huduma, Miongozo yetu ya Jumuiya, Sera yetu ya Tathmini kwa mujibu wa Masharti yetu ya Huduma. Iwapo kutakuwa na ukiukaji unaorudiwarudiwa au mbaya sana, tunaweza pia kuzuia, kusimamisha au kuondoa akaunti husika ya Airbnb.
Ikiwa unaamini kwamba maudhui yanakiuka sera hii, unaweza kuripoti maudhui hayo moja kwa moja kupitia programu au kwa kuwasiliana nasi.