Iwe wewe ni mtaalamu wa ukarimu mwenye uzoefu, au umeanza kukaribisha wageni, ni muhimu kuelewa jinsi kodi zinavyokufaa. Kama mwenyeji, kulingana na eneo lako, unaweza kuhitajika kukusanya kodi za eneo husika, Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) au kodi ya Bidhaa na Huduma (GST) kwenye ukaaji wako, tukio au bei ya huduma kutoka kwa wageni wako.
Katika baadhi ya maeneo, Airbnb inaweza kukusanya na kutuma kodi fulani kwa niaba yako. Hata hivyo, kunaweza kuwa na kodi nyingine unazowajibikia. Ukiamua kwamba unahitaji kukusanya kodi za ziada, ni muhimu kwamba wageni wajulishwe kuhusu kiasi halisi cha kodi kabla ya kuweka nafasi.
Ikiwa ukusanyaji na ulipaji wa kiotomatiki wa Airbnb haupatikani kwa kodi fulani, unaweza kukusanya kodi mwenyewe.
Kulingana na nchi unayoishi, huenda ukahitaji kutoa hesabu ya VAT/GST kwenye ofa unayotoa. Tunakuhimiza uwasiliane na mshauri wa kodi katika mamlaka yako ili upate ufahamu zaidi au ikiwa unahitaji usaidizi wa kutathmini VAT/GST kwenye huduma unazotoa.
Aidha, Airbnb inahitajika kukusanya VAT/GST kwenye ada zake za huduma katika nchi ambazo zinatoza kodi kwa njia ya kielektroniki. Angalia taarifa zaidi kuhusu jinsi VAT inavyofanya kazi kwa ajili ya sehemu za kukaa , matukio na huduma.
Kulingana na aina ya kodi iliyokusanywa, inaweza kuwa na maelezo ya kina tofauti katika ripoti yako ya kodi.
Ikiwa unastahiki kukusanya kodi mahususi kupitia kipengele chetu mahususi cha kodi, kodi hizo zinakusanywa kutoka kwa mgeni na kutumwa kwako kama njia tofauti ya malipo ya kodi. Unawajibikia kuwasilisha, kulipa na kuripoti kodi zote mahususi zinazohusiana na nafasi ulizoweka kwa mamlaka husika za kodi.
Ripoti yako ya kodi itakusanya kodi zako mahususi kwa kila nafasi iliyowekwa, kuzilipa pamoja kama kitu kimoja, na kujumuisha maelezo ya nafasi iliyowekwa kama vile jina la tangazo na msimbo wa kuweka nafasi, pamoja na kiasi cha jumla kilicholipwa. Malipo yako yanajumuisha bei yako ya kila usiku, ada ya usafi na ada nyingine zozote unazokusanya kwa ajili ya uwekaji nafasi mpya, bila kujumuisha ada ya huduma ya mwenyeji.