Ikiwa unahitaji kumrejeshea mgeni fedha kwa ajili ya huduma au tukio, unaweza kufanya hivyo kupitia uzi wa ujumbe.
Ikiwa mgeni ataghairi ndani ya kipindi chako cha kughairi, atarejeshewa fedha kiotomatiki ndani ya siku 10 za kazi, kwa hivyo huhitajiki kufanya chochote.
Ikiwa mgeni yuko nje ya kipindi chako cha kughairi, atahitaji kughairi nafasi aliyoweka na kukutumia ombi la msamaha. Una saa 24 za kuamua ikiwa unakubali ombi na kisha kumrejeshea mgeni fedha.
Mara baada ya nafasi iliyowekwa kughairiwa, kalenda yako inafunguliwa na fedha zinarejeshwa kwa mgeni. Hakuna athari kwa wenyeji kwa ajili ya ughairi huu.